To save content items to your account,
please confirm that you agree to abide by our usage policies.
If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account.
Find out more about saving content to .
To save content items to your Kindle, first ensure no-reply@cambridge.org
is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings
on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part
of your Kindle email address below.
Find out more about saving to your Kindle.
Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations.
‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi.
‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.
Decolonization in East Africa was more than a political event: it was a step towards economic self-determination. In this innovative book, historian and anthropologist Kevin Donovan analyses the contradictions of economic sovereignty and citizenship in Tanzania, Kenya and Uganda, placing money, credit, and smuggling at the center of the region's shifting fortunes. Using detailed archival and ethnographic research undertaken across the region, Donovan reframes twentieth century statecraft and argues that self-determination was, at most, partially fulfilled, with state monetary infrastructures doing as much to produce divisions and inequality as they did to produce nations. A range of dissident practices, including smuggling and counterfeiting, arose as people produced value on their own terms. Weaving together discussions of currency controls, bank nationalizations and coffee smuggling with wider conceptual interventions, Money, Value and the State traces the struggles between bankers, bureaucrats, farmers and smugglers that shaped East Africa's postcolonial political economy.
Utii ni amri moja katika amri kubwa za Mungu, tena amri yenyewe ina maana kubwa kabisa. Adamu na Hawa walitakiwa kutii. Hapana ujinga mkubwa katika maisha kama kufikiri kwamba mtu aweza kuishi bila utii wowote.
Kwa ajili ya kuendesha vema sheria au maisha lazima pawe na utii. Utii ni kazi ya kudumisha amri mahali pa machafuko. Kuna utii wa mwili na wa akili. Mwili ulioadabishwa, kama askari, hutii amri kama mashine. Akili iliyoadabishwa haishikwi na hasira ghafula. Hatuwezi kufunzwa utii na wengine siku zote. Lazima tujifunze sisi wenyewe.
Utii ndiyo njia bora ya kuweka msingi kwa ubora kwa wakati ujao wa mtoto. Lazima afunzwe kutii wazee na walimu wake, kuamka na kulala bila kuchelewa, kujifunza masomo yake na kutakasa mwili wake. Kuna wazee waharibuo watoto kwa kuwaruhusu kutenda lolote wapendalo kwa sababu ya mapenzi. Wadhani kwamba utii ni utumwa, namna ya neno litazamiwalo kwa watumishi. Lakini si utumwa. Ni adili ya kutengeneza uhuru wa mtoto. Mtoto asiyeadabishwa atakuwa mtu mwenye fujo ya mawazo na matendo ya ujinga.
Utii una maana kubwa sana katika madaraka au sheria. Kazi ambayo watumishi wake huja wakatoka wakati wowote wapendao, itajiona katika orodha ya kufilisika mara moja. Skuli, ambayo walimu na wanafunzi huja wakati wowote wapendao, yachekesha sana kufikiri. Utii si udhalimu. Jeshi bila utii huwa kama kundi la watoto watukutu. Hadithi hutwambia kwamba jeshi la askari milioni moja wasioadabishwa hushindwa upesi na jeshi la askari elfu tano walioadabishwa. Kwa hivyo, utii ni sehemu kubwa ya mafundisho ya jeshi. Kosa dogo la utii huadhibiwa kwa ukali.
Katika maisha ya raia na utawala wa nchi, utii hufaa sana. Serikali huongoza utawala kwa msaada wa kikosi kidogo sana cha polisi au askari. Lakini hufaulu, kwa sababu ya utii. Toka kwa Gavana mpaka kwa mtumishi mdogo kabisa, kila mtu hutii amri, lao si kuuliza kwa nini, ila ikipasa, kutenda au kufa. Kwa hivi utii hupasa kwa serikali. Hupasa vile vile kwa kila jamii ya watu.
Kuandika kwa chapa ni uvumbuzi uwezeshao mtu yeyote kusema na umati mzima juu ya neno afikirilo kuwa muhimu, na uwezeshao nchi nzima kusikiliza maneno ya mtu kama huyo, kadiri alivyo mkubwa au mdogo, kwa urahisi na makini makubwa ya kuelewa asemayo kuliko mtawala Mwafrika anavyohutubia kabila katika baraza yake. Hatibu aweza kusema na watu waliopo, lakini kitabu kilichopigwa chapa hakisemi na kabila liliopo tu, ila husema na vizazi vyote vinavyofuata kikampatia na sifa mwandishi wake.
Tarehe ya kuvumbuliwa kuandika kwa chapa haijulikani hasa, lakini ikikadiriwa huwezekana kusemwa kwamba ni uvumbuizi wa karne ya kumi na tano. Caxton aliyeanzisha kiwanda chake mwenyewe cha kuandika kwa chapa akapiga chapa vitabu, husemwa kwamba ndiye mvumbuzi wa kuandika kwa chapa. Kuandika kwa chapa katika zama za kwanza kulikuwa si kwepesi wala hakukuwa wazi. Lakini kuandika kwa chapa kwa sasa ni ajabu ya kazi ya mashine.
Uvumbuzi wa kuandika kwa chapa umefanya maongozi makubwa sana katika hali zote za maisha. Kwa neno zima, uvumbuzi huu umeleta mageuzi makubwa kabisa katika ulimwengu. Kuandika kwa chapa ni uti wa malezi na elimu ya sasa. Hata katika karne ya kumi na tano uvumbuzi huu uligeuza maisha ya dini na nchi, kwa kufanya watu kujisomea wenyewe, badala ya kutengemea mashehe. Hivyo haki ya mashehe ya kumiliki elimu yote peke yao ilitanguka elimu ikawa miliki ya kila mtu.
Kuandika kwa chapa kulileta ufufuo wa elimu Ulaya. Zamani vitabu viliandikwa vikatunzwa katika miswada. Nakala nyingine zilipotakiwa, mtu ilimpasa kunakili kitabu kizima kwa mkono. Lakini kwa majilio ya kuandika kwa chapa idadi yoyote ya nakala huwezekana kupigwa chapa, na thamani ni ndogo. Maskini waweza kununua vitabu watakavyo. Elimu husafiri kila mlango. Maandiko huwa rahisi. Wakati na nguvu itumiwayo katika kunakili vitabu huokoka. Kwa hiyo kuandika kwa chapa kumesaidia sana maendeleo ya elimu.
Hifadhi ya msichana ni jambo kubwa, hasa ipasapo mwanamume kutoa shauri. Walakini bahari kuu huvukwa. Kwa hivi ninatumaini kuwa sitazama katika jaribu hili.
Msichana wa leo ni mama wa kesho. Upumbavu ulioje kujifanya hatudhuriwi na mambo yake! Ukitaka kukomesha maisha yetu ua wasichana, na baada ya miaka si mingi hapatakuwa na kitu kiitwacho mtu. Robo tatu za hifadhi hii lazima, zifanywe na wanaume.
Msichana akipita balehe akafikia utu uzima hufanya mvuto mkubwa kwa mwanamume. Mvuto huu ni maumbile, na pana watu wadaio hapana maana ya kugombana na maumbile. Nataka ningeona kama waonavyo wenzangu; lakini watu wote hawana vipawa namna moja. Kinyume cha maono yao, naona halali kugombana na tokeo hili kwa sababu pengine mvuto huu humponza msichana.
Kama yapasa msichana kujitafutia riziki kwa utumishi kama uyaya, uuguzaji au ualimu; tena kama akikaa pasipo wazazi wake hukutana na majaribu mengi ya wanaume. Vikundi vya wanaume humzunguka kama nzi kando ya kipande cha sukari. Humganda kama nyuki juu ya tone la asali.
Kwa msichana aliyelelewa vema majaribu haya hayadhuru. Onyo la busara la mama likitolewa mapema ni ngao bora kwa msichana kuliko buibui jeusi, dirisha la komeo au mlango wa kufuli. Kwa bahati mbaya wasichana wengi hawapati malezi mazuri. Hawa lazima waokolewe. Wakiokoka watasaidia kuhimiza majilio ya Afrika bora. Hatutaki Afrika kuwa bora?
Msichana akijitolea ovyo katika tamaa ya mwili huharibikiwa na mambo yake mengi. Huingia katika hatari ya maambukizo ya maradhi mabaya. Hasara nyingine ya kusikitisha ni uzazi wa haramu. Kwa hali ya kiitikadi iliyo katika maisha yetu ya sasa, ni dhiki kubwa kwa msichana kupata mtoto asiye baba wa kusaidia ulezi wake. Moja lolote katika haya likitokea huharibu heshima ya msichana. Hufukuzwa kazini, hapati arusi njema na dunia nzima humdharau. Matokeo haya mabaya sana, nayo yote huletwa na wanaume wajinga na walafi.
Isifikiriwe kuwa wanaume wote waovu. Hasha mara mia. Wanaume wengi wema nao wana heshima. Hawana nia ya kuharibu maisha ya msichana hata kidogo. Fahari yao kubwa katika maisha ni kuwasaidia.
Ni bora tuendelee kuishi au tustahabu mauti? Swali hili gumu sana. Tungeendelea kuishi tukasikiliza kwa uvumilivu usio mpaka misiba yetu, au tungejitahidi kupigana na misiba hata kwa mauti mashaka yakapata kukoma kututesa? Mauti na usingizi ni kama maumbu. Hapana tofauti kubwa iwezekanayo kuonekana kati yake. Kama katika usingizi twasahau mashaka yetu ya mchana, kadhalika katika lepe la mauti, tutatupilia mbali uzito wa mashaka ya maisha. Faraja kama hiyo, kitulizo, au njia kama hiyo ambayo kwayo twaweza kuepuka mashaka yasiyohesabika ya maisha, ni ajabu kubwa na ipendezayo mno. Walakini, kama katika usingizi, majinamizi au ndoto za kutaabisha hutokea mara kwa mara, kadhalika mfano, katika mauti huenda pakatokea ndoto ambazo hapana mtu hata mmoja azijuaye. Hofu ya kuzimu kuna nini kubwa sana katika mioyo yetu.
Kama mauti ni faradhi yamekadiriwa kwa kila mtu. Kama ni deni limepasa watu wote kulipa. Pasipo shaka sisi sote tutakufa, wala hatutaweza kurudi katika maisha kama tuamkavyo katika usingizi wetu wa kila siku. Hofu hii ya mambo yasiyojulikana katika mauti ndiyo itufanyayo tutake kuendelea kwa taabu kuchukua uzito wetu wa huzuni katika maisha.
3. Furaha haihusiani na maisha ya mjini wala shamba
4. Furaha halisi ni furaha ya moyo
Watu mbalimbali wana mawazo mbalimbali ya furaha. Wengine huvutwa na maisha ya shamba kwa sababu ya amani na wastani wake, na wengine huvutwa na maisha ya mjini kwa sababu ya uzuri, fahari na anasa zake. Wengine wadhani kwamba furaha huletwa na utajiri, wakati wengine wadhanipo kwamba furaha halisi hupatikana katika umaskini.
Sidhani kwamba tajiri ana furaha halisi, kwa sababu ana fedha ya kununulia atakacho tu. Fedha haiwezi kununua kila kitu. Fedha huleta uwezo, faraja na furaha, lakini ina mipaka yake vile vile. Kwa mfano, fedha haiwezi kununua urafiki wa kweli, au mapenzi ya kweli, amani au furaha halisi. Fedha yaweza kununua dawa bora kabisa dukani, lakini haiwezi kununua afya. Wakati huo huo, sidhani kwamba maskini ni mtu mwenye furaha halisi. Ni dhana tupu tu kufikiri kwamba kila mkulima ni mtu mwenye furaha, na kila mtu akaaye katika kibanda hulala usingizi mnono. Mwulize mkulima tu aonavyo utaona mambo yalivyo. Washairi na wataalamu zamani walitukuza umaskini lakini kweli ni kwamba furaha halisi huihusiani na utajiri wala umaskini.
Katika utafiti wetu wa furaha tutaona kwamba furaha ya kweli huja kwa akili yetu wenyewe. Twaweza kuhuzunika hata wakati tumekaa juu ya mlima wa dhahabu na kufurahi hata kama hatuna senti moja ya shaba mifukoni mwetu. Nadhani kwamba furaha ya kweli huja tuwapo si matajiri wala maskini, lakini tuweze kutimiza haja na faraja zetu zipasazo katika maisha tu. Maisha ya raha hutia uvivu na ulegevu. Nadhani furaha ya kweli huja kwa kuzifanyia kazi haja zenyewe, lakini si kwa kuwa na choyo.
Wengine huona furaha kwa kuishi kama mkulima katika shamba. Maisha ya shamba yana nafuu nyingi juu ya maisha ya mjini kwa sababu ya haraka ya ovyo na makusudio yake mbalimbali. Katika kijiji kuna amani na neema. Lakini kwenda kijijini hakugeuzi mtu mwenye huzuni kuwa mtu mwenye furaha usiku mmoja. Mtu aweza kupata amani hata katikati ya mji juu ya makelele na ghasia zake za desturi kama pana amani katika moyo wake.
Palitokea shindano la wanawake juu ya kueleza uzuri wao katika nchi ya hewa ya manukato, ardhi ya kioo mito ya marashi na makonde ya mapambo. Nchi hiyo ilikuwa ndoto kubwa ya wanawake kwa sababu kila mwanamke alijali sana manukato na mapambo kuliko wakati wake, tena alipenda sana kioo kuliko kazi yake. Washindani walikuwa Mnene kwa ajili ya wanawake wanene, Mwembamba kwa ajili ya wanawake wembamba, Mweupe kwa ajili ya wanawake weupe, na Mweusi kwa ajili ya wanawake weusi. Kwa kuwa silaha kubwa ya mwanamke ilikuwa ulimi wake, kila mshindani alikuwa msemaji mwema katika shindano
Mnene alijitangaza, “Katika wanawake wazuri ulimwenguni hapatikani mwanamke wa kushindana na mimi. Angalia, nina afya na nguvu! Uzuri wa kwanza mwilini ni afya, nami ninayo ya kutosha. Kwa nguvu yangu, naweza kufanya kazi yoyote ngumu itakiwayo. Mimi ni fahari ya wanawake katika dunia.”
Mwembamba alinena, “Uzuri wangu haulingani na wa mwanamke yeyote katika dunia hii ya haraka na wepesi. Wembamba si udhaifu. Ni umbo la ajabu liwezalo kutenda miujiza bila kutoka jasho. Nina wepesi na haraka katika matendo yangu. Baadhi ya kazi hutaka akili, nami ninayo kwa wingi. Mimi ni bora katika mabibi.”
Mweupe alisema, “Mimi ni nuru katika wanawake kama jua lilivyo katika mbingu na dunia. Jua mfalme wa sayari, binti yake ni mimi. Kwa hivi uzuri wangu haushindwi na wa mwanamke yeyote. Nashika macho ya ulimwengu mzima katika mkono wangu mmoja. Furaha ya dunia imo katika miliki yangu.”
Mweusi alitamka, “Mimi ni bora katika wanawake. Weusi si uchafu. Ni aina moja ya maumbile, nayo ina uzuri wake. Kwa weusi wangu nimekuwa taji juu ya kila kichwa cha mtu. Ukitazama katika nywele, nyusi, kope na mboni za macho ya watu utaona rangi yangu. Kurasa za vitabu vikubwa duniani zimeandikwa kwa wino mweusi. Mimi ni malkia wa uzuri katika wanawake.”
Kama ulikuwa mmoja wa waamuzi katika shindano hili, ungalimpa ushindi mwanamke gani?
Uwezo wa magazeti :— Magazeti yana uwezo kamili juu yetu. Ulimwengu hutegemea sasa maono ya magazeti. Uongo kidogo huweza kupotoa fahamu za elfu za watu, na kuzuia kweli makusudi kukaweza kutumbukiza nchi nzima katika ukatili na maangamizi yasiyo mpaka. Tunaishi katika karne iliyotawaliwa kabisa na magazeti.
Kazi zake katika nyakati za vita na amani :— Yana uwezo mkubwa katika amani na vita. Yaweza kukuza au kupunguza matisho ya vita. Yaweza kuongoza nchi katika vita au amani. Makala yasiyo hadhari yaweza kutia nchi katika moto wa vita. Kwa hivi lazima yafanye kazi yao kwa hadhari na heshima.
Taarifa nyofu na imara :— Kazi yake ya kwanza ni kuarifu kwa unyofu na makini. Yasiwe na mapendeleo ya itifaki au baadhi fulani. Yasihofu kufanya mapatilizo ya nguvu bila ya chuki yoyote. Yasihofu kupatiliza hata serikali kwa ajili ya manufaa bora ya watu. Serikali zote zenye busara huruhusu uhuru wa magazeti. Yasitumie uhuru wake kwa kusingizia yakaharibu sifa au majina ya watu.
Gazeti mwalimu mkubwa :— Watu wengi sana husoma magazeti tu, kwa kutenda hivyo huweza kukuza akili zao. Kwa mtu wa kawaida gazeti ni rafiki, kuhani na nwongozi. Ni njia ya kueneza elimu za namna zote. Kwa hivi daraka lake ni kubwa sana. Lazima lisitawishe upeo, akili na maarifa ya watu. Lisidunishe hali hii kwa makala hafifu na matangazo ya dawa za kudhuru na bidhaa mbovu.
Ubora wake :— Ni msingi wa historia ya taifa katika wakati ujao. Kwa hivyo, lazima yatoe mambo yaliyo sahihi kama iwezekanavyo.
Kazi yake :— Kwa kuwa uwezo na daraka lake ni kubwa, kazi yake ni kuwa nyofu kwa kuwa na haki na kweli katika kila neno lisemalo.